3/15/2019

Tambo za Zitto Kabwe kufuatia mtanange wa Simba SC na AS Vita Club kesho


Ikiwa kesho Simba SC wanaingia katika mtanange na Timu ya AS Vita Club pale uwanja wa Taifa, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambaye ni shabiki ndaki ndaki wa timu hiyo amesema kesho ni siku muhimu kwao.

Zitto amewataka mashabiki wote wa timu hiyo nchini na Watanzania wote wafurike uwanjani ili kuwapa nguvu vijana wa Timu hiyo.

"Kesho ni siku muhimu sio kwa @Simba SC Tanzania na mashabiki wake tu bali kwa Taifa zima. Nawasihi mashabiki wote wa Simba nchini na Watanzania wote tufurike uwanjani ili kuwapa nguvu Vijana wetu. WaKongo lazima walale. Ushindi wa Simba ni Ushindi wa Tanzania 🇹🇿 dhidi ya DRC," ameandika Zitto kupitia ukurasa wake Twitter.