3/17/2019

Uongozi wa Yanga SC watoa tamko baada ya kufungwa na Lipuli FC


Baada ya kupoteza mchezo wake wa jana kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Samora mbele ya Lipuli Uongozi wa Yanga SC umefunguka kuwa bado kazi inaendelea kwani kukosa ushindi ni sehemu ya matokeo.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa bado wana nafasi ya kuendelea kupata matokeo kwenye michezo inayofuata kikubwa ni mashabiki kuendelea kutoa sapoti.

"Tumepoteza mchezo hatujapoteza matumaini, bado tuna nafasi ya kuendelea kufanya vizuri na kupata matokeo chanya mashabiki mtupe sapoti," amesema Ten.

Mchezo wa jana unakuwa wa tatu kwa Yanga kupoteza baada ya kuanza kupoteza mbele ya Stand United, Simba na Lipuli na kufanya wabaki nafasi ya kwanza na pointi zao 67.