3/17/2019

Vanessa Mdee ahudhuria Mkutano wa kimataifa wa Crans Montana


Pamoja na kuwa mwanamuziki aliyefanikiwa sana, muimbaji Vanessa Mdee anajihusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kijamii. 

Leo hii yupo kwenye Mkutano wa kimataifa wa Crans Montana Forum unaofanyika mjini Dakhla, Morocco. Anaiwakilisha taasisi yake ya Udada Foundation ambayo lengo lake ni kumpigania mtoto wa kike.

Utakumbuka August mwaka jana Vanessa kupitia Foundation yake hiyo aliwapatia zawadi ya mtambo maalumu wa umeme wa nguvu ya jua (sola) kutoka kampuni ya Zola shule ya wasichana ya Arusha girls.