Vifo vya wamama wajawazito vyapungua kwa zaidi ya 40%


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wadau wa masuala ya Afya imefanikiwa kupunguza Vifo vya wamama wajawazito kwa zaidi ya 40% , hali inayotokana na uboreshwaji wa huduma za Afya kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu jana wakati wa ufunguzi wa jengo la wagonjwa wa kulipia hospitali ya CCBRT Jijini Dar es salaam.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imejenga na kuboresha zaidi ya vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya 350 ambavyo vinatoa huduma za dharura ikiwemo huduma ya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni.