Vijana watakiwa kuchangamkia fursa


Na. Timothy Itembe, Mara 

Mbunge wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara, Lameck Airo amewataka vijana kuchangamkia frusa za maendeleo pindi zinapojitokeza badala ya kushinda siku nzima wakipoteza mda mwingi kwenye mitandao ya kijamii huku wakichati.

Airo alisema jana katika kikao cha Baraza la vijana kilichokalia Ukumbi wa CCM Utegi kilicho washirikisha Mbunge pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya Rorya,Charles Ochere kilichokuwa kikijadili mpango kazi wa mwaka 2019/2020 kutoka kata hadi wilaya wa UVCCM.

Airo alisema kuwa vijana waliowengi hawataki kufanya kazi pamoja na kuchangamkia frusa zinapojitokeza badala yake wanashinda siku nzima wakichati kwenye mitandao bila kujua kuwa wanapoteza mda mwingi wa kufanya shuguli za maendeleo.

Airo  alitumia nafasi hiyo kumpengeza Rais John Pombe Magufuli kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 na kutekeleza miradi mbalimbali kwa wananchi wake ambapo kwa nafasi hiyo Wanachama wa Chama cha mapinduzi kwa sasa wanatembea kifua mbele bila kuogopa wapinzani tofauti na kipindi kilichopita.

Mbunge huyo aliongeaza kuwa katika halmashauri yake ya Rorya wamepokea fedha shilingi milioni 625 kutoka serikalini kwaajili ya utekelezaji wa elimu bure ambazo fedha hizo zitaenda kugawanywa na  kusaidia maendeleo ndani ya  Shule mbalimbali za sekondari zilizopo Rorya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Wilaya Rorya,Charles Ochere alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Serikali ambao wanadriki kutumia fedha za serikali vibaya kwahali hiyo alitumia nafasi hiyo kuwataka Viongozi wenye tabia hiyo kuacha mara moja kwani Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli hapendi tabia kama hiyo badala yake anapenda viongozi wanaowatumikia wananchi

Naye katibu wa Chama hicho wilaya Rorya,Lucey Boniphas alimpongeza Mbunge wa jimbo la Rorya,Lameck Airo katika kuhakikisha zoezi la kuandikishaji wanachama linaloendelea la uandikishaji wanachama kwajia ya Elektroniki linafanikiwa ambapo alitoa  fedha zake za mfukoni kwaajili ya kununulia  Simu mbili za sumatphone  zenye dhamani ya zaidi shilingi milioni tatu ili kufanikisha zoezi la uandikishaji wanachama.