https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wananchi watakiwa kuongeza nguvu na kasi katika uzalishaji wa zao la muhogo | Muungwana BLOG

Wananchi watakiwa kuongeza nguvu na kasi katika uzalishaji wa zao la muhogo


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi nchini kuongeza nguvu na kasi katika uzalishaji wa zao la muhogo kutokana na zao hilo kuwa na soko la uhakika kwa kuwepo kwa ongezeko la Viwanda vinavyochakata Unga wa muhogo.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo mapema leo alipokuwa anazindua kiwanda cha kisasa cha kuzalisha unga wa muhogo cha kampuni ya ulimaji na usindikaji muhogo Tanzania (Cassava starch of Tanzania Corparation - CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kata ya Nyengedi Mkoani Lindi.

Aidha Waziri Majaliwa ameeleza kuwa muhogo ndio zao pekee lenye kustahimili mabadiliko ya hali ya hewa na kuwataka wananchi kutilia mkazo katika uzalishaji wa zao hilo kutokana na uhitaji mkubwa ulioko kwa uanzishwaji wa kiwanda hicho.