Wanawake waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wailalamikia Mahakama


Na, Clavery Christian; Bukoba.

Katika uzinduzi wa kampeini ya muungano wa utepe mweupe nchini wanawake mkoani kagera wamelia kutotendewa haki pindi wanapokwenda mahakamani kushitaki vitendo wanavyofanyiwa na waume zao nyumbani na jamii kwa ujumla.

Bi, Jamarati Chrizostom ni muhanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kutumia mabavu na Mme wake ambaye amempelekea kupata majeraha na kuugua kutokana na kupigwa na kuuchomwa na kisu na mda mwingine kushikiwa panga kutaka kumuua.

Amesema kuwa wanawake wengi wanaonyanyaswa kijinsia na kufanyiwa vitendo vya ukatili wanashindwa kwenda mahakamani kwasababu wanapofikisha kesi zao mahakamani mahakama inawaachia huru watuhumiwa na kurudi mtaan na kuanza kuwatishia amani wale wanaokuwa wamewashitaki mda mwingine kuwavizia na kuwapiga.