Watalaam wa Figo kutoka Japan kuzidi kuzuru Tanzania


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu Afya) Dkt.Zainabu Chaula amekutana na kufanya mazungumzo na wataalam kutoka Shirika la Tokushukai nchini Japan ambao walifika nchini kwa ajili ya kupandikiza figo (Renal Transplant) kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Katika Mazungumzo hayo wamekubaliana kuwa na mpango endelevu wa kuleta wataalam wao kwenye Hospitali hiyo na vilevile wataalam wa Benjamin Mkapa kwenda kupata ujuzi nchini Japan.

Katika awamu hii wagonjwa watatu wamefanikiwa kupandikizwa figo na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa saba kufanyiwa tangu huduma hiyo ianze kutolewa katika Hospitali hiyo iliyopo jijini Dodoma.