Aachana na mchumba wake kisa dola elfu 10


Binti mmoja huko nchini Kenya ambaye jina lake limehifadhiwa kakubali kumuacha mchumba wake baada ya kupewa pesa na wazazi wa mchumba wake yaani wakwe zake watarajiwa.

Wazazi wa mchumba wa mwanamke huyo wamempa pesa hizo ambazo ni dola elfu 10 sawa na milioni 23 za kitanzania kwa masharti yakuachana na mtoto wao,kwa madai kuwa mwanamke huyo sio chaguo zuri kwa mtoto wao.

Lakini mwanamke huyo alibainisha sababu zilizomfanya apokee pesa zile kwanza wazazi wa mwanaume kutokumkubali,lakini pia kitendo cha mwanaume huyo kubadilika sana baada ya kumchumbia pia vilimtatiza kwani alikuwa akimfuatilia kupita kiasi kwa kutaka kujua kila anakoenda ,na aligundua kuwa mwanaume huyo ni mlevi kupindukia na akilewa anafanya vitu vya ajabu.