ACT Wazalendo wasalimu amri kwa Polisi, wasitisha maandamano


Ngome ya Vijana Chama cha ACT Wazalendo wamesitisha maandamano yao waliyopanga kuyafanya hapo kesho mkoani Dodoma hadi April 9 mwaka huu.

Mapema leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto aliwatahadharisha wananchi wote waliopanga kufanya maandamano siku ya kesho kushinikiza Bunge kufanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assaad kuwa wasithubutu kufanya hivyo kwani watapigwa hadi watachakaa.