https://monetag.com/?ref_id=TTIb ADC kufanya mkutano mkuu na kuwachagua viongozi | Muungwana BLOG

ADC kufanya mkutano mkuu na kuwachagua viongozi


Na Thabit Hamidu, Zanzibar.

Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema kinatarajiwa kufanya  mkutano  mkuu Zanzibar  ifikapo aprili 14  mwaka huu ambapo katika mkutano huo wanachama watapata fursa ya kuwachagua viongozi wapya watakao ongoza chama hicho kwa kipindi kijacho.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa  Sanaa  Raha leo Mjini Magharib Unguja, Mwenyekiti wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo alisema katika  mkutano huo mkuu utahusisha na uchaguzi  ambapo wanachama watachagua viongozi kama sheria, kanuni na taratibu za chama hicho kinavyosema.

Alisema katiba ya chama hicho kinatoa fursa ya kufanyika kwa uchaguzi kila inapofika kipindi Fulani hivyo katika mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar utatoa fursa ya  wanachama kuwania nafasi mbali mbali.

“Chetu kinaongozwa na katiba na kusimamiwa na taratibu mbali mbali ambapo tuna mfumo  wa kufanya uchaguzi ambapo wanachama wanatakiwa kuchukua form na kuwania nafasi hizo,


Si kila siku chama kinaongozwa na viongozi haohao kwetu sisi kila mwanachama anahaki ya kugombania nafasi ya uongozi na kuongoza Chama”alisema Doyo hassani Doyo.

Alisema mbali na uchaguzi katika mkutano huo kunatarajiwa kuzinduliwa mpango mkakati wa chama hicho ambapo unatarajiwa kutekelezwa na wanachama wa chama hicho takribani wote Tanzania nzima( bara na visiwani).

“Mpango mkakati huo una lengo lake nikuchangia maendeleo ya chama hicho ifikapo 2020 katika uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo alibainisha kuwa katika mkutano huo kutafanyika marekebisho ya sheria kwa baadhi ya vipengele katika katiba yao ambavyo vina upungufuna kuto endana na hali ya kisiasa ya hivisasa Nchini.

“miongoni mwa vipengele hivyo ni vipengele vya vikundi vya ulinzi na vipengele vingine ambavyo tumeona vina mapungufu katika katiba yetu”alisema