Loading...

4/17/2019

Aliyehamia CCM kutoka CHADEMA azua gumzo bungeni


Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Getrude Ndibalema ambaye siku ya jana alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) amezua gumzo kwa dakika kadhaa baada ya kutambulishwa Bungeni.

Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge alimtambulisha Getrude kwa kutumia maneno “aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu BAVICHA” jambo ambalo Wabunge wengi wa CHADEMA walionekana kupinga wakisema “tulimfukuza huyo” lakini wabunge wa upande wa CCM walionekana kumshangilia.

Leo Bunge linajadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Loading...