Aliyekuwa katika kikosi cha U - 17 cha Guinea afariki Dunia


Nyota kinda wa aliyekuwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Guinea Aly Soumah amepoteza maisha akiwa nchini kwao Guinea saa chache baada ya kupata ajali ya gari akiwa njiani kuelekea kwao.

Aly Soumah aliyepoteza maisha akiwa angali na umri mdogo, alikuja nchini Tanzania kwa ajili ya fainali za AFCON U-17 zinazofanyika nchini Tanzania lakini kwa bahati mbaya ndoto yake ya kushiriki fainali hizo ilizimwa mapema kabla hata ya mchezo wao wa kwanza.

Nafasi ya kinda huyo kucheza fainali hizo ilizimwa baada ya CAF kuwafanyia wachezaji hao vipimo vya mwisho vya uhakiki wa umri wao kutumia kipimo cha MRI lakini nyota huyo akaonekana kuzidi umri, hivyo akalazimika kurudishwa kwao Guinea kabla hata timu yake ya Guinea haijacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Cameroon.