.

4/15/2019

Azam FC kuifuata Ndanda FC kibabe


Uongozi wa Azam FC, umeeleza kuwa kwa sasa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Ndanda FC baada ya kuinyoosha Mbeya City jana.

Azam FC walifanikiwa kushinda kwenye Uwanja wa Sokoine mbele ya Mbeya City kwa bao 1-0 lililofungwa na Yakub Mohammed.

Kupitia kwenye ukurasa wao wa Istagram wa Azam Football Club, umeeleza kuwa Baada ya kuzoa pointi tatu dhidi ya Mbeya City jana, kikosi cha Azam FC tayari kimerejea jijini Dar es Salaam leo mchana, kabla ya kesho Jumanne asubuhi kuanza safari nyingine ya kuelekea mkoani Mtwara kukipiga na Ndanda.

Azam FC wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 66 baada ya kucheza michezo 31.