Benki Kuu ya Sudan yaamuliwa kuchunguza uhamishaji wa fedha


Baraza la Kijeshi linaloongoza Serikali ya mpito nchini Sudan limeiamuru Benki Kuu ya nchi hiyo, kuchunguza shughuli zote za uhamishaji wa fedha zilizofanyika kuanzia Aprili 1, na kushikilia fedha zote zinazotiliwa shaka.

Hayo yameripotiwa leo na shirika la habari la Sudan SUNA, Baraza hilo pia limeamuru kusimamishwa kwa shughuli ya kubadilishwa umiliki wa hisa, hadi itakapotangazwa vinginevyo.

Benki Kuu vile vile imeamuliwa kuripoti kwa mamlaka husika, juu ya kufanyika mchakato wowote wa uhamishaji mkubwa wa fedha au unaotiliwa shaka ya hisa pamoja na umiliki wa makampuni.