https://monetag.com/?ref_id=TTIb Bodi ya Ligi yaja na maamuzi kuhusu viporo vya Simba SC | Muungwana BLOG

Bodi ya Ligi yaja na maamuzi kuhusu viporo vya Simba SC


Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura ameeleza kuwa watafanyia kazi viporo vya Simba ambavyo vimezidi kuwa vingi kutokana na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa.

Wambura ameyasema hayo kufuatia mjadala ambao unazidi kushika kasi dhidi ya viporo hivyo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinatajwa kupunguza ladha ya ligi.

Kiongozi huyo amesema wataandaa ratiba maalum ya Simba ili wacheze mechi hizo ili kuendana na kalenda ya TFF ilivyopanga kuwa ndani ya mwezi Mei wanataka ligi iwe imemalizika.

Amefunguka kuwa kuna fainali ya Kombe la Shirikisho 'FA' ambalo pia mshindi bado hajapatikana nalo fainali yake inapaswa kucheza.

Moja ya watu waliolalamikia Simba kuwa na viporo vingi mpaka sasa ikiwa na 11, ni Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye alieleza kama kuna upendeleo fulani unafanyika.