Golikipa aliyevunjika mguu aongezewa mkataba na kutibiwa bure


Klabu ya Horoya AC ya nchini Guinea imempa kipa wake Khadim N'diaye (34) mkataba wa miaka 3 na itagharamikia mafunzo yake ya ukocha atakapostaafu, baada ya kipa huyo Kipa huyo kuvunjika mguu kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca na anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita.

N’diaye alivunjika mguu kwenye mchezo warobo fainali ya klabu bingwa Afrika mchezo uliomalizika kwa Horoya kufungwa mabao 5-0 .

Golikipa huyo aliumia vibaya wakati alipotoka langoni kujaribu kumzuia mshambuliaji wa Casablanca alisifunga na kujikuta akigongana na mlinzi wake na kupelekea kuvunjika mguu. Khadim N’Diaye anatarajiwa kurudi uwanjani baada ya miezi sita akiwa na nguvu na uenda huu ukawa sio mwisho wa kucheza soka