https://monetag.com/?ref_id=TTIb Hakuna mimba zinazotokea gerezani - Waziri Lugola | Muungwana BLOG

Hakuna mimba zinazotokea gerezani - Waziri Lugola


Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amesema kuwa hakuna mimba zinazotokea gerezani bali wafungwa wanaojifungua huingia nazo.

Ameeleza hayo Bungeni leo katika kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge Khatibu Haji alihoji juu ya wanawake kupata ujauzito wakiwa ndani ya Gereza wakati walinzi wao ni wanawake wenzao.

"Hakuna mimba zinazotokea gerezani, mimba tunazozungumzia ni ambazo mfungwa aliingia nazo akiwa gerezani, ndiyo maana kulitokea jaribio kwa Wabunge tupitishe sheria wenza wa wabunge waende gerezani ili kufanya mapenzi lakini hatutakubali jaribio hilo." amesema Waziri Lugola.

Ameendelea kwa kueleza kuwa, 'Na tumekuwa na utaratibu,watoto ambao wamezaliwa magerezani kwanza wanapofikia umri wa kuanza elimu ya awali, wamekuwa wakisoma katika shule za awali za magereza yetu'.