Haya ndio mambo ambayo wasichana waliopo single wanatakiwa kuyafahamu

Mwanamke unapokuwa single isiwe kigezo chako cha kulaumu mambo ambayo yanakufanya ufike mahali mpaka unakufuru, yawezekana upo single kwa sababu ya mazingira ambayo wewe mwenyewe unajiweka katika mazingira hayo, hivyo unapokuwa single yafutayo ndiyo mambo ya msingi unayopaswa kuyazingatia:

1. Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.

2. Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi.

3. Kuangalia namna ya uvaaji wa mavazi yako na mwonekano wako mbele ya jamii…. Usitegemee kuvaa kimini ukutane na mwanaume wa suti… wewe utampata wa milegezo na kubana pua tu.

4. Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.

5. Usimsubiri mwanaume mpaka aje  ndiyo uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.

6. Tengeneza mazingira ya kuilinda afya yako.

7. Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe.

8. Usitumie sex kama ndio mzani wa mapenzi.Unaweza ukaachika tuu pamoja na penzi lako tamu.

9. Usiolewe na mtu kwa sababu ya fedha, Utabakia kuwa mtumwa wake.

10. Jiongezee ubora wako, Tafuta kazi. Usiwe mpuuzi ukaamini mwanaume atatatua matatizo yako yote.