https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kim Kardashian apata ofa ya kazi | Muungwana BLOG

Kim Kardashian apata ofa ya kazi


Mwanasheria mashughuli Marekani, Robert Shapiro amempa ofa ya kazi Kim Kardashian kwenye kampuni yake ya masuala ya sheria, ikiwa zimepita siku chache tu tangu Staa huyo wa Reality show kutangaza kuwa anataka kuikamilisha ndoto yake ya kuwa mwanasheria.
.
Wiki chache zilizopita Kim Kardashian alitangaza kuwa ameamua kufata nyayo za Baba yake mzazi na tayari ameanza kuingia darasani kusomea uanasheria, Pia hivi karibuni alishiriki kwenye mipango wa kubadilisha sheria za Magereza Marekani na pia alikutana na Rais Trump kushinikiza mabadiliko na vilevile tayari pia amesaidia watu kadhaa kupata uhuru.
.
Robert Shapiro amesema atampa kazi iwapo atafaulu mtihani wake wa Uanasheria, Shapiro alikuwa mtu wa karibu wa Baba yake Kim, Robert Kardashian ambaye pia alikuwa mwanasheria na walifanya kazi pamoja kwa ukaribu kwenye kesi kubwa ya OJ Simpons miaka ya 90.
.