Kocha wa Simba SC atoboa siri ya kuwachapa Coastal Union


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema mchezo wao wa jana dhidi ya Coastal Union ulikuwa mgumu kutokana na uwanja ulivyokuwa.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-1 na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.

“Haikuwa rahisi sababu uwanja haukuwa mzuri lakini tulifanikiwa kumiliki mchezo na baadae tulifanya mabadiliko ambayo yametuletea magoli, kubwa zaidi ni ushindi,” amesema kocha huyo.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kikosi cha Simba SC kilirejea Dar es Salaam mara moja kwa maandalizi ya mchezo unaofuata.