https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kocha wa Yanga SC alalamika kuhusu waamuzi wa Ligi Kuu | Muungwana BLOG

Kocha wa Yanga SC alalamika kuhusu waamuzi wa Ligi Kuu


Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa katika mechi walizofungwa msimu huu idadi kubwa zimechangiwa na maamuzi mabovu ya marefa wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliochezesha mechi zao. .

Kocha huyo amesema endapo kungekuwa na haki katika michezo yao basi wangekuwa wamejihakikishia Ubingwa mpaka sasa.

"Unajua mimi nimezunguka nchi nyingi sana Afrika lakini sijawahi kuona maamuzi ya hovyo kama ya waamuzi wa Ligi ya Tanzania, Hakuna haki na kungekuwa na haki nina uhakika sasaivi tungekuwa tushajihakikishia ubingwa." alisema Zahera

Zahera amesema kwasasa anajipanga kwenye michezo inayofuata ukiwemo wa Azam ili kuhakikisha anashinda mechi zote zilizosalia.

Aidha , Kocha huyo amesema atahakihakikisha anatwaa ubingwa wa Kombe la ASFC ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.