Korea ya Kaskazini yafanya jaribio la silaha


Korea ya Kaskazini imesema imefanya jaribio la silaha nyengine mpya na wakati huo huo kuitaka Marekani kumuondoa Waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo katika mazungumzo ya baadaye ya Nuklia.

Jaribio hilo ambalo halikuonekana kama limekiuka masafa yaliyopigwa marufuku ya makombora ya nuklia imeliruhusu taifa hilo kuonyesha kwamba linaendelea na kutengeza silaha za nuklia na vile vile kuwahakikishia wakuu wa jeshi la nchini humo kuwepo kwa ishara za udhaifu wa kidipolomasia na Marekani.

Mchambuzi kutoka eneo la Korea Kazkazini alisema taarifa zilizoko katika vyombo vya habari katika taifa hilo zinatoa ishara ya kwamba silaha iliyojaribiwa ni kombora jipya ambalo linaweza kushambulia bara moja hadi jengine.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya mambo ya Marekani katika wizara ya masuala ya kigeni ya Korea Kazkazini, ilimshutumu Pompeo kwa kudharua matamshi muhimu ya rais Kim Jong Un na vile vile kupuuza matakwa ya Korea Kazkazini ya kutaka mazungumzo ya Nuklia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Taarifa hiyo ilimtaja Pompeo kama mtu wa kubuni mambo wakati katika hotuba yake siku ya Jumatatu alipopinga kauli ya Kim ya makataa ya mazungumzo ya Nuklia aliposema angependa mpango huo kukamilika hivi karibuni.

Korea Kazkazini inasema kuendelea kwa Pompeo kuwa katika mazungumzo hayo ni kuhakikisha kwamba mazungumzo hayo yanakorogeka hivyo basi kuitaka Marekani kumbadilisha na mtu mwengie aliye makini zaidi na mweledi wa mawasiliano.