Kwa haya yaliyofanywa na COMPASSION hakika serikali inapaswa kuwapongeza


Na. John Walter, Babati

Ili mtoto aweze kutimiza ndoto zake lazima jamii ishiriki kikamilifu kuweza kumsaidia katika kumpatia elimu bora,chakula na mahitaji muhimu ya binadamu pamoja na kuheshimu mawazo yake.

Shirika la COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA (CIT) limeishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuvifufua,kuviendeleza na kujenga viwanda vipya ili kuwa na uchumi wa viwanda utakao inua na kuboresja maisha ya watanzania wote.

Wametoa pongezi hizo walipokuwa wakisheherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo hapa nchini  April 1999,sherehe ambazo mkoani Manyara zimefanyika katika mji wa Babati na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Hanang  Joseph Mkirikiti.

Aidha  wameiomba serikali ifanyie kazi mapungufu ambayo ni kikwazo kinachowakabili katika kufikia kupata elimu bora ikiwa ni ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi hasa katika shule za sekondari,upungufu wa madarasa kwa shule za awali na msingi kulingana na matakwa ya sera ya taifa,upungufu wa vitabu pamoja na kutokuwepokwa vifaa vya kutosha katika maabara za shule.

Pamoja na hayo watoto/vijana hao wametumia maazimisho hayo kupinga ajira za watoto katika maeneo ya mbalimbali ikiwemo viwandani,mashambani,Migodini,majumbani na hata mitaani na kuiomba serikali ikishirikiana na wazazi/walezi kuwanasua wapate haki yao ya eli ikiwa ni pamoja na kuwapenda,kuwajali na kuwalinda.

Mkuu wa wilaya ya Hanang Joseph Mkirikiti  akizungumza katika sherehe hizo mjini Babati,amesema serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli bado inaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopo katika sekta ya elimu ili kuhakikisha inatoa elimu bora kwa watanzania wote.

Amesema yeye yupo tayari kuwatumikia watoto muda wote atapoambiwa na kwamba anachukia sana vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali kushindwa kuhudhuria kwenye sherehe za watoto haswa ambazo hazina Malipo akiwaita kuwa ni Watumishi wa posho,wa Ovyo.

 Kauli mbiu ya maazimisho hayo ya miaka 20 ya shirika la Compassion hapa nchini,Wekeza kwa watoto na vijana kwa uchumi endelevu.

Wamesema kuwa inalenga katika kumwandaa mtoto/kjana wa kitanzania kufikia na kufaidi matunda ya uwepo wa uchumi huo ambao utampatia maisha bora.

Aidha shirika hilo katika kuhakikisha kuwa inampatia elimu bora mtoto/kijana  imeweka vipaumbele katika kuwajengea uwezo watoto na vijana katika kujifunza fani mbalimbali za kiufundi wawapo katika shughuli za kiprogramu vituoni  ikiwa ni pamoja na useremala,ushonaji wa nguo na viatu,uchomeleaji wa vyuma,utengenezaji wa matofali ya Block na Kadhalika, na hukutana  kila jumamosi .

Makanisa Ambayo Yameingia Ushirika Wenza Na Shirika La Compassion International Tanzania Yakiwa Na Lengo La Pamoja La Kumkomboa Mtoto Kutoka Kwenye Umaskini Kwa Jina La Yesu,kwa upande wa Mkoa wa Manyara Ni Kkkt Babati Mjini,Anglikana Nakwa,Elim Pentecoste Babati ,Anglikan Sing Na ,Fpct Babati.

Shirika kwa miaka 20 tangu lilipoanza rasmi mwaka 1999 limefanikiwa kufikia malengo na utume wa Compassion na Kanisa kwa kuwafungua watoto na vijana kutoka vifungo vya umaskini wa Kiroho,Kijamii,Kimwili na Kiuchumi ambayo yanadhihirishwa na vijana ambao kwa sehemu kubwa wamefika katika hatua mbalimbal za mafanikio.

Baadhi ya watoto/vijana waliohudumiwa na shirika hilo wanasema kama sio huruma ya Mungu kupitia ufadhili huo wasingeweza kupata elimu na kufika hapo walipo kwani wazazi wao hawakuwa na uwezo wa kulipia gharama za elimu wala matibabu.

Hata hivyo shirika linamhudumia mtoto tangu utotoni hadi anapofikisha umri wa kuweza kujitegemea miaka ishirini na mbili [22].

Historia ya shirika hilo inaonyesha kuwa lilianzishwa miaka 67 iliyopita wakati mchungaji Everett Swanson alipokuwa safarini kutoka mjini Chicago kuelekea Korea ya Kusini mnamo mwaka 1952 ili kuwafikishia injili wanajeshi wa Kimarekani waliokuwa wakipigana vita nchi Korea Kusini.

Mchungaji Swanson akiwa anafanya shughuli zake huko ndipo alipoanza kuhangaishwa na moyo wa Huruma baada ya kushuhudia mamia kwa mamia walio achwa yatima  mitaani kutokana na kutelekezwa na jamii zao.

Anasema siku moja asubuhi alishuhudia gari la kubeba taka likizoa taka mtaani ambapo kwa mbali aliona likinyanyua mzigo mzigo wa uchafu wa matambara yaliyochakaa,lakini aliposogea karibu na gari hilo aligundua kuwa zile taka taka hazikuwa matambara bali ilikuwa ni miili ya watoto yatima waliopoteza maisha kwa usiku mmoja ,hatua iliyompelekea yeye kudhamiria kufanya kitu kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa aina hiy.

Mwaka 1953 aliamua kuanza kampeni za uchangisha fedha za misaada na mwaka uliofuata alianzisha program ya ufadhili ya kuwasaidia watoto yatima kwa kiasi kidogo cha dola kwa mwezi.

Ilipofika mwaka 1963 Mchungaji Swanson alitiwa moyo na maneno ya Yesu kutoka katika kitabu cha Mathayo 15:32 yasemayo “Yesu akwaita wanafunzi wake,akasema nawahurumia mkutano,kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami,wala hawana kitu cha kula,tena kuwaaga wakifunga sipendi,wasije wakazimia njiani.” Na huruma hiyo kwa Yesu katika mstari huu ndiyo iliyozaa jina la COMPASSION kwa kiingereza likiwa na maana ya “HURUMA”kwa Kiswahili na ndipo mwaka 1980 ikazaliwa COMPASSION INTERNATIONAL na makao yake makuu ni Colorado Springs nchini Marekani na utume mkuu wa shirika ukawa ni Kuwafungua watoto kwenye umaskini kwa jina la Yesu.

Mwezi April 2019 shirika hilo linatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake,ambapo kwa kuanzishwa kwake imeyaletea fursa makanisa mengi ya kiinjili ya kuweza kuwahudumia watoto na vijana mbalimbali wanao kabiliwa na hali ya umaskini,na mpaka sasa limefanikiwa kuanzisha vituo 454 katika mikoa 19 nchini yenye jumla ya watoto wapatao laki moja [100,000].