4/17/2019

Lulu atangaza ujio wake kwenye filamu


Msanii wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amesema yupo mbioni kurejea rasmi kwenye ulingo wa filamu.

Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds FM amesema kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha ujio wake huo.

"Kwenye movie nitarudi hivi karibuni, nahitaji kukua sehemu zote, sio tu kwenye maisha yangu bali hata kwenye kazi zangu na vitu vingine. Nipo kwenye process ya kurudi kwenye movies na itachukua muda kurudi kwa sababu nataka utofauti na vile nilivyokuwa navifanya zamani kwenye movies," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Kiukweli kwenye tasnia ya filamu tumeyumba kwa kiasi fulani na hata ukiangalia uzalishaji wa filamu umepungua sasa kama uzalishaji umepungua hata ushirikishwaji wa tuzo za filamu kwa nchi zingine umepungua, Tupo kwenye wakati wa kuboresha tasnia yetu hivyo nina imani mambo yatakuwa sawa mbeleni'.