Maswali ya kujiuliza ili kupata mafanikio

Wakati mwingine hautaji nguvu nyingi katika kusakamafanikio, ila unahitaji akili za kufikiri ili kuyapata hayo mafanikio. Ukishapata hayo mafanikio ndipo unapohitaji nguvu nyingi katika kufanya kazi. Inawezakana ukawa hajaniekewa, ngoja nikueleweshe ni kwamba kila kitu kinaanza na kufikiri hapa ndipo wazo linapoanza kutengenezwa. Wazo hilo likishakamilika ndipo unapohitaji nguvu katika kufanya kazi.

 Mpenzi msomaji wa makala hii siku ya leo  tutangalia katika kujua umuhimu wa kufikiri ili kupata mafanikio. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika ya kuwa watu wengi tumekuwa na maisha yalele ambayo yanatufanya tusisonge mbele kimafanikio hii ni kwa sababu tumekuwa tunafikiri mambo ya kawaida sana.

Mambo ambayo unahitaji kujiuliza ili kupata mafanikio;

1. Unataka kuwa na nani?
Hili ni swali la muhimu sana la kujiuliza uwe unayetaka mafanikio zaidi. Mfano wewe ni mwanafunzi wakati unasoma katika masomo yako je umewahi kujiuliza unataka kuwa na nani katika maisha yako ya hapo baadae? pia na wewe mfanya biashara katika maisha yako umewahi kujiuliza unataka kuishi maisha gani? je biashara yako unataka iweje baada ya miaka kadhaa? je unataka kuwa hapo ulipo au unataka kuwa mfanyabishara mkubwa au mdogo?

Ukishajiuliza maswali hayo lazima ujiuulize tena sifa hizo unazo au huna? na kama huna sifa hizo unazipata wapi. Ewe unayesoma makala haya shusha pumzi kisha twende sawa hebu jione upo  mahali baada ya muda fulani ndoto zako zimetimia. Kimsingi ni kwamba hayo yote yanakupa nafasi nzuri ya kujua malengo yako na kujua ni kitu gani ambacho unakihitaji katika maisha yako.

2.Unataka kutatua matatizo yapi?
Kwenye kutatua matatizo ndipo pesa zilipo. Unashangaa wala usishangae pia haujakosea kusoma. Ulimwengu wa leo ni ulimwengu wenye matatizo mengi ambayo yanahitaji majibu na mtoa majibu ni wewe. Unatoa macho ndio wewe ndiye mtoa majibu ya changamoto zinazowakabili watu. Badilisha mkao uliokaa kisha tuendelee, aliyegundua facebook leo hii katatua tatizo la watu na kutukutanisha watu pamoja na kuifanya dunia kuwa kinganjani mwako na tunafurahia maisha hayo, mtu huyo leo ni miongoni mwa watu matajiri ulimweguni kwa sababu aliweza kusoma mazingira na kuona watu tuna changamoto yeye akaja na changamoto.

Kutatua changamoto za watu hauhitaji mifano kutoka kwa wazungu ila kila jambo unalotaka kulifanya kumbuka liwe linatoa majibu ya changamoto ya watu. Wewe unayefanya biashara ya kuuza chipsi endelea na kazi hiyo maana unasaaidia unatatua tatizo la njaa kwa haraka zaidi, kitu cha msingi ongeza ubunifu katika kazi yako ili kuongeza wateja wengi zaidi. Huo ni mfano tu ila kumbuka kutatutua matatizo ya watu ili kupata pesa.

Hadi kufikia hapo afisa sina la ziada, kitu cha msingi  cha kukumbuka ni kwamba endelea kufuatilia makala za kimafanikio ili uweze kufanikiwa zaidi.

Na; Benson Chonya