Mbunge wa CCM na CUF warushiana vijembe Bungeni


Mbunge wa Jang’ombe, Ali Hassan King na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji wamerushiana vijembe bungeni na kusababisha wabunge kuangua vicheko.

Vijembe hivyo vilizuka mapema leo, wakati wabunge wakichangia Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bungeni Dodoma leo ambapo wakati Khatib akichangia alisema yeye ameenda kufanya kazi bungeni na kama King ameenda kuimba na kucheza taarabu ni yeye.

Baada ya kusema hivyo, ndipo King naye akapata nafasi ya kuchangia na kusema  mchicha una mwiba lakini unaliwa kama Khatib akitaka kuimba taarabu atumie kipaza sauti anachotumia yeye sio zake nyingine anazotumia mtaani.

Hata hivyo, haikueleweka wabunge hao walikuwa wanamaanisha nini lakini imekuwa ni kawaida kwao kurushiana vijembe pindi mmojwapo anapopata nafasi ya kuchangia ama kuuliza swali bungeni.