.

4/15/2019

Mfahamu mwanaharakati Sir Isaack Newton


Sir Isaack Newton (25 december 1642 – 20 march 1726) Alikuwa ni mwana fizikia, mwanahisabati, mwanateolojia na mwanafalsafa asilia  ambaye amekuwa ni ufunguo muhimu katika ulimwengu wa kisayansi.

Newton aliweza kuvumbua kanuni ya mwendo, kanuni nguvu ya mvutano na nyingine nyingi. Sir Isaack Newton alizaliwa 25/12/1642 siku ambayo ilikuwa ni siku ya krismas, alizaliwa miezi mitatu baada ya kifo cha baba yake ambaye alikuwa ni mkulima mwenye mafanikio makubwa aliyejulikana pia kwa jina la Isaack Newton.

Sir isaack newton alizaliwa njiti jambo ambalo lilipelekea kukua akiwa na siha mbaya lakini mama yake alimlea katika mazingira mazuri ambayo yalimkuza newton bila kushambuliwa na magonjwa. Akiwa na umri wa miaka 3 mama yake aliolewa kwa mara ya pili na akaenda kuishi kwa mume wake mpya aliyejulikana kwa jina la Reverend Barnabas Smith ambapo alimwacha Newton mikononi mwa Mkunga mmoja aliyejulikana kwa jina la Margery Ayscough.


Akiwa kijana isaack hakumpenda baba yake wa kambo na akajenga uadui dhidi ya mama yake kwa kuolewa na baba huyo hata akadiriki kutoa kauli kuwa angeweza kuwachoma kwa moto wote ndani mpaka wafe. Mama yake Newton alipata watoto watoto watatu kutoka kwenye ndoa yake ya pili na inasadikika Newton hakuwahi oa mpaka mauti ilipomchukua 20/03/1726.

Akiwa na umri wa miaka 12 Newton alianza masomo yake kwenye shule ya kifalme iliyojulikana kwa jina la Grantham ambapo ilikuwa ikifundisha kilatini na sio hisabati baada ya muda mfupi aliondolewa kwenye shule hiyo na akashinikizwa na mama yake walejee kwenye shughuli za kilimo kama baba yake lakini Newton aliichukia sana hiyo kazi, Henry Stokes ambaye alikuwa mwalimu wa Newton alimshauri mama yake Newton kumrudisha kijana wake shuleni ili akamilishe masomo yake, mama yake alikubali na baada ya kurudi shuleni Newton alifanya vizuri kwenye masomo yake na akaongoza kwa muhula ule.


Mwezi juni 1661 alijiunga na chuo cha Utatu Cambridge kwa shinikizo la mjomba wake Rev Willium Ayscough ambapo alihitimu mwaka 1664, kwa wakati huo Newton alisoma masomo yaliyohusu  Aristotle,  wakati mwingi alionekana na notebook iliyokuwa imejaa maswali mengi yaliyohusu Falsafa ya kimakanika.

Mwaka 1665 alifanikiwa kugundua binomial theorem na akaendelea kugundua kanuni za kihisabati. Muda mfupi baada ya Newton kuhitimu digrii BA 1665, chuo kilifungwa kwa muda ikiwa kama ishara ya awali kwa chuo kuporomoka kitaaluma.

Newton aliendelea kujisomea akiwa nyumbani na taratibu alianza kuona mafaniko katika nadharia za mahesabu na sheria ya Mvutano. Mnamo april 1667 alirudi chuoni Cambridge na mwezi oktoba alichaguliwa kama mwana Utatu, ambapo kazi yake ilikuwa ni kuhubiri.

Kazi ya Newton ilikuwa kupanua uwezo wake katika nyanja zote za kimahesabu na ndoto yake ilitimia sawia ambapo akawa mwalimu wa hisabati na somo lake lilijulikana kama fluxions au calculus, kazi ambayo ilionekana rasmi mnamo mwaka 1669 katika muswada ambao ulitolewa kwenye magazeti mbalimbali katika mwaka huo.

Mnamo mwaka 1669 mwalimu wa Newton aliyejulikana kwa jina la Isaack Barrow, alimwandikia barua John Collins mwezi August ikisema[ Newton ni mwanafunzi wangu ambaye ana uwezo mkubwa wa kiakili (genius)ambaye sijawahi kuona}.

Baadaye Newton aliingia mgogoro na Leibniz ambaye pia alikuwa ni mwanahisabati na mwanafalsafa mjerumani Mgogoro huo ulitokana na mgongano wa kimaendeleo wa sayansi ya kimahesabu kwa wakati huo, Historia inasema Leibniz alitanguliwa kuvumbua kanuni nyingi za kimahesabu ambazo alianza kuzitoa rsmi na kuanza kutumika mwaka 1684 zaidi ya Newton ambaye kanuni zake zilitolewa mwaka 1693, bado inaendelea kufafanua kuwa pamoja na kwamba Leibniz alitangulia kuvumbua kanuni za kimahesabu na ambazo nyingi leo hii zinatumika kwenye nchi za Ulaya, lakini bado kwenye vitabu vyake alishindwa kuunda kanuni ya Calculus ambayo ni Newton pekee ndiye aliyeidhihirisha kwenye vitabu vyake pekee, na ni ambayo inaonekakana kwenye kitabu chake cha kwanza kilichoitwa Newton’s principia itself kilichotolewa mwaka 1687 na baadaye akatoa kitabu kingine kilichoitwa de motu corporum in gyrum ( on the motion of bodies in orbit) na kanuni yake calculus Newton alichelewa kuitoa rasmi kutokana na kuogopa utata na upinzani uliokuwepo kipindi hicho miongoni mwa wanasayansi.

Baadaye akawa rafiki mkubwa wa Nicolas Fatio de Duillier hiyo ikiwa ni mwaka 1691 Duillier alianza kuandika kitabu cha pili (new virsion) cha Newton Principia na mahusiano ya kanuni za Leibniz ambapo ilikuwa ni mwaka 1693, lakini kitabu hakikukamilika kwasababu mahusiano ya yeye na Newton yalififia ghafla.


Kuanzia mwaka 1699 ulizuka mgogoro mkubwa sana kati Newton na Leibniz ambapo wafuasi wa Newton walimtuhumu Leibniz kuwa amenakili masomo na kanuni za Newton, lakini baadaye ilikuja dhihirika kuwa ni Newton ndiye aliyeandika masomo yaliyohusisha hotuba za Leibniz jambo ambalo liliendelea kuzua utata kitu kilichopelekea uhai wao kuwa mashakani, na baadaye Leibniz alifariki 1716 na bado kifo chake kilihusisha mgogoro uliokuwepo baina yake na Newton.

Newton alipopata masters akawa mwalimu wa Utatu Usiogawanyika ambayo ilikuwa ni 1667, na alikula yamini kuwa atajikita kwenye theolojia kama somo lake kuu na atafanya shughuri za kimungu pale atakapopata amri toka kwa viongozi wake wa dini. Kwa kipindi hicho mwalimu yeyote wa chuo cha Cambridge alilazimika kuwa mtumishi wa dini yaani muhubiri au padre katika kanisa la Angricana.

Newton aliwahi kuwa mbunge katika nchi ya Uingereza kupitia jimbo la chuo cha Cambridge 1689-90 na 1701-2 na baadaye akawa kansela wa masuala ya fedha. Uchumi wake ulikuja kuporomoka kwa kasi mara baada ya kampuni yake ya bahari ya kusini, ilipokufa. Kampuni hiyo ilikuwa ikijihusisha na biashara ya watumwa, alipoteza takribani dola za Uingereza elfu ishirini.

Karibu kabisa na mwisho wa maisha yake Newton alihamia Cranbury Park karibu na Winchester akiwa na familia ya mpwa wake na akaishi huko mpaka mauti yalipomkuta mnamo 20/03/1727, mpwa wake Catherine Barton Conduitt alimpenda sana mjomba wake na alimsaidia sana tangu alipoanza kuugua mpaka kifo chake, enzi za uhai wa Newton, Newton mwenyewe aliwahi kumwandikia barua mpwa wake juu ya upendo mkubwa kwake muda mfupi baada ya kupona ugonjwa wa ndui. Newton alifia usingizini usiku wa kuamkia 20, machi, 1727 huko london Uingereza na akazikwa Westminster Abbey.

Mara baada ya kifo chake nywele mwili wake ulichunguzwa kwa makini na baadaye iligundulika kuwa nywele zake zilikuwa na asili ya mercury.


Mwisho ni kwamba kazi ya sir isaack Newton imekuewa ni kielelezo cha masomo mengi ya sayansi ulimwenguni kote, hii ni juhudi na maarifa ya mtu mmoja pekee ambaye anakumbukwa na ataendelea kukumbukwa na vizazi vijavyo.