Mfanyabiashara atatua changamoto ya uhaba wa vyoo shuleni


Na Clonel Mwegendao

Shule ya Msingi Tumaini iliyopo kata ya Binagi Wilayani Tarime Mkoani Mara inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa Matundu ya Vyoo 40  kufuatia changamoto hiyo wadau wa Maendeleo wameombwa kujitokeza kusaidia ili kutatua changamoto hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Fidel Mahende ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Gwisana kata ya Binagi  kipindi akipokea Msaada wa Mifuko ya saruji 50 kutoka kwa Richard Matiko ambaye ni mfanyabiashara na mzaliwa wa kata hiyo ili kuongeza nguvu za wananchi katika ujenzi wa Matundu ya vyoo kwa lengo la kutatu achangamoto hiyo.

Fidel alisema kuwa Shule ya Msingi Tumaini kwa sasa inamatundu 12 ya vyoo lakini bado nayatoshi kwa idadi ya wanafunzi zaidi ya 800 hivyo pungufu sasa ni matundu 40 ambapo alitumia fursa hiyo kuomba wadau wote waliosoma shule mama Nyameigura ambayo imezaa Tumaini waweze kuchangia ili kusaidia shule hiyo.

"Shule ya Tumaini ni Mpya sasa imezaliwa na shule mama Nyamwigura na hivi vyoo matundu 12 wamepatiwa na shule mama shule mpya haina vyoo ndo maana wazazi wameanza kuchimba shimo hili kwa lengo la ujenzi wa Matundu ya vyoo ili kusaidia watoto wetu" alisema Mahende.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji Nyamwigura Paul Magere aliongeza kuwa   licha ya changamoto ya matundu ya vyoo katika shule ya Msingi Tumaini bado kuna upungufu wa vyumba vya madarasa hivyo ameiomba serikali kuwaunga mkono ikiwa ni pamoja na kuezeka maboma ambayo wameisha jenga kwa nguvu zao.

"Mwaka jana hii shule mama ya Nyamwigura iliezuliwa na upepe sasa tumejitaidi na kujenga maboma 16 bado ahayajaezekwa tunaomba serikali itusaidie kuezeka ili kupunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika hizi shule mbili Tumaini na Nyamwigura" alisema Paul.

Richard Matiko ni Mfanyabaishara Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mkazi wa kata ya Binagi  alisema   kuwa ameguswa na changamoto ya  upungufu wa Matundu ya Vyoo katika shule ya Msingi Tumaini nakuamua kutoa Mifuko50 ya Saruji ili kupunguza changamoto huku akiomba wadau wengine kumuunga mkono.

"Mimi kama kijana na mfanyabiashara mdogo na mzalendo wa nchi yangu ya Tanzania nimeguswa sana na changamoto ya upoungufu wa matundu ya vyoo kwa sababu hata matundo yaliyopo kwa sasa siyo rafiki nimeona kwa kidogo nilichobarikiwa niweze kujitoa na wadau wengine wanawezakujitoa ili tusaidie jamii yetu" alisema Richard.

Aidha Matiko aliongeza  kuwa mifuko hiyo ya saruji itawapunguzia hadha wanayoipata wazee na watu wasiojiweza kipindi cha makundirika yanavyopita majumbani  kuwasaka wananchi ili washiriki maendeleo mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa shule, Zahani na Miundombinu Mingine.

"Nimekuwa nikiona maeneo yetu ya huku vijijini wazee na watu wasiojiweza wanakamatiwa mali zao kwa sababu ya kushindwa kushiriki suala la Maendeleo sasa msaada wangu huu wa Mifuko 50 ya Saruji wenda ikawa suluhu ya kuwasaidia kwa kiasi kidogo" alisema Matiko.

Changamoto ya upungufu wa matundu vya vyoo katika shule ya msingi Tumaini inaonekana kwa sababu ni shule mpya ambayo imetokana na shule mama nyamwigura hivyo kwa sasa shule hiyo inatumia vyoo vya shule mama ambapo sasa wananchi wameanza kuandaa miundombinu ili ujenzi wa matundu uanze mara moja.