Mtoto afanyiwa ukatili kwa kuloweka uyoga mwingi kwenye maji



Na Amiri kilagalila-Njombe

Mama mmoja  aliyefahamika kwa jina la Letisia Lisulile mkazi wa mtaa wa Igangindung'u kata ya Kivavi amefikishwa katika kituo cha polisi  makambako kwa kosa la kumpiga na kumfunga mikono na miguu kwa kamba na mpira mtoto wake mwenye umri wa miaka saba anaye soma darasa la pili shule ya msingi magegele  kwa madai ya kuloweka uyoga mwingi kwenye maji.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo uliopo kata ya Kivavi mjini makambako Emmanuel Gadau amesema  tukio la kupigwa kwa mtoto huyo na kufungwa kwa mpira akiwa uchi si mara ya kwanza kufanywa na mama huyo bali amekuwa akiwafanyia watoto wake ukatili huo mara kwa mara.

"mimi ndio niliomsaidia kumkata mtoto hiyo kamba kufungua kwa mkono nilishindwa nikatumia kisu kukata kamba huku mtoto analia jinsi kamba ilivyombana na sio kamba peke yake ulitangulia mpira,na huyu kumpiga sio mara ya kwanza anapiga watoto wake mara kwa mara na mimi siwezi kuvumila na anampiga mtoto kisa uyoga"alisema Mwenyekiti

Baadhi ya majirani wa mama huyo wamesema kuwa wamechoshwa na tabia za mama huyo kwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili watoto wake kila wakati na pindi wanapomshauri amekuwa akiwapa maneno ya kashfa.

"Tulishuhudia mtoto alivyopigwa huku mikono imevimba yaani huyu mwanamke mwenzetu sijui ni wa aina gani, tunashukuru mtoto huyu alikurupuka na kukimbia yaani huyu mama sitaki hata kumsikia kwasababu ni mara nyingi na ukienda pale umuulize ana maneneo ya kashfa"walisema majirani

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba mwanafunzi wa shule msingi darasa la pili amesema kuwa mama yake alimfunga kwa kamba mikononi na miguuni na kuanza kumpiga kwa fimbo,kisu na panga kwa kosa la koloweka uyoga ambao alitaka kuupika.

"Nilikuwa nimeloweka uyoga mama akasema kwanini umeloweka wote nikasema nilitaka kuupika ndio akanifunga mikononi na miguuni akachukua kisu,fimbo na panga ndio akaanza kunipiga"alisema mtoto

Naye mama wa mtoto huyo Letisia Lisulile amekiri kumpiga mtoto huyo, na kueleza kuwa amekuwa akiwapeleka shambani kulima asubuhi kwa kuwa baba yao hatoi pesa za  kuwalelea watoto hao.

"yaani ilikuwa kama ni hasira kwasababu mara nyingi anakimbilia mitaani na nikimuuliza akasema babaake ndio alimwambia akiona namuadhibu awe anakimbilia kwa mama ake mkubwa,na babaake siishi naye na huwa hasaidii kutoa chochote katika malezi ya watoto huwa nahangaika mwenyewe"alisema Letisia

Kwa upande wake Baba wa mtoto huyo Japhet Mwalongo amesema kuwa awali alikuwa na wake watatu na baada ya kuokoka akaacha nao wawili na kubaki na mke mmoja lakini pesa za matumzi amekuwa akitoa kwa watoto wote.