https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mvua iliyokwama Tanzania yawasili Kenya | Muungwana BLOG

Mvua iliyokwama Tanzania yawasili Kenya


Mvua iliyodaiwa kukwama Tanzania hatimaye imeanza kunyesha Kenya kwa kasi, huku wananchi wakiwa hawajajiandaa.

Wafanyabiashara waliokuwa wamepanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara za jiji la Nairobi wameshindwa kufanya shughuli zao kutokana na mvua hizo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, saa mbili kabla ya mvua hiyo kunyesha, idara ya hali ya hewa Kenya ilitangaza kuwa mvua itanyesha jijini Nairobi na maeneo mengine.

''Sikutarajia kwamba itanyesha na nilipokuwa nikiendelea na biashara yangu ilianza kunyesha  nikalazimika kutafuta hifadhi kwengineko,'' amesema mfanyabiashara mmoja nchini humo.

Wiki iliyopita naibu mkurugenzi wa idara hiyo, Bernad Chanzu alisema hakutakuwa na mvua msimu huu.

Wiki mbili zilizopita idara hiyo ilitangaza kuwa kiangazi kitaendelea mwisho wa mwezi huu huku mawingu ya mvua yakisalia Tanzania kutokana na kiwango cha chini cha upepo wa kusukuma mawingu hayo kuelekea Kaskazini mwa nchi hiyo.