Nchi 30 zapiga sheria ya kuwapiga mawe hadi kufa mashoga


Nchi zaidi ya 30 ambazo zinaongozwa na Canada, zimeomba Brunei kufuta adhabu ya kifo iliyopitishwa hivi karibuni dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na adhabu nyingine kali.

Muungano kwa Haki sawa (CDE) ulielezea katika taarifa ya mwishoni mwa wiki hii iliyopita "Masikitiko yake makubwa" baada ya uongozi wa nchi hiyo kupitisha "adhabu kali" chini ya sheria mpya ya jinai kulingana na sheria za dini (Sharia).

"Tunahimiza serikali ya Brunei kufuta hukumu mpya na kuhakikisha kwamba hatua yoyote iliyopitishwa inaendana na sheria za kimataifa za haki za binadamu," taarifa hiyo imeeleza.

Mbali na kupigwa mawe kwa watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja au uzinzi, sheria hiyo mpya ya jinai ya Brunei pia inaruhusu kukatwa mkono au mguu mwizi.