https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ni aibu CCM kuwa na kiongozi anayedhalilisha Wanawake - Mbunge Peneza | Muungwana BLOG

Ni aibu CCM kuwa na kiongozi anayedhalilisha Wanawake - Mbunge Peneza


Upendo Peneza ambaye Mbunge wa viti Maalumu (CHADEMA) amemtuhumu Katibu Mwenezi kwa CCM, Humphrey Polepole kuwa anadhalilisha wanawake kwa kauli zake kuhusu wabunge wa Viti Maalumu.

Peneza ametoa kauli hiyo wakati, Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2019/20, Peneza amesema kuwa wabunge wa viti maalumu wapo kwa mujibu wa Katiba na nashangazwa na kauli zinazotolewa na Polepole.

“Kitu kibaya kinachoendelea ndani ya nchi hii, kilianza ndani ya Bunge hili lakini Mwenyekiti na viongozi wengine walikemea tabia hii ya “kipuuzi”, lakini sasa imefika huko nje ambapo ndugu, Humphrey Polepole amesema wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wanapatikana mpaka “wapitiwe” na Mwenyekiti wao, huu ni udhalilishaji,” amesema Upendo Peneza.

“Sasa kama hata hatambui haki za kikatiba ni aibu kwa Chama cha Mapinduzi kuwa na mwenezi anayedhalilisha wanawake,”amesema Peneza na kuendelea “Ifike mahali nafasi walizonazo na vyeo walivyo navyo viheshimiwe. Ni aibu kwa kiongozi wa nchi hii kusimama na kusema kwamba mafanikio ya mwanamke ya kisiasa yanatokana na shughuli za kingono, tunawajengea watoto wetu fikra mbaya ndani ya Vichwa vyao“.

Peneza anadai kuwa Polepole anasema kuwa ‘Wabunge wa Viti Maalumu CHADEMA hawapiti mpaka wapitiwe na Mwenyekiti wao," Alisema bila kuweka wazi ni wapi Polepole alitoa kauli hiyo.