NIC yatoa msaada kwa Wilaya ya Ilemela


Na. James Timber, Mwanza

Shirika la Bima la Taifa( NIC) limetoa msaada wa mifuko  270 ya saruji  hii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika suala zima la kukuza na kuboresha elimu h nchini.


Akiwasilisha msaada huo wenye thamani ya milioni 5.4 mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Sam Kamanga amesema kutoa msaada huo ni kuunga mkono dhana ya utawala bora katika suala zima la kurudisha katika jamii kile kinachopatikana kutokana na shughuli za shirika lao

Amesema kwamba wao kama shirika kwa sasa wamejikita zaidi kusaidia katika sekta ya elimu  na afya hapa nchini.

Akipokea hiyo ya saruji,Mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Angelina Mabula ameshukuru shirika hilo kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika wilaya.

Mabula alisema kwa kusema kama wilaya bado wana uhitaji mkubwa wa kujenga madarasa ya kutosha kulingana na idadi ya ufaulu mkubwa wa wanafunzi wa darasa la saba.

 Alisema wameanza zoezi la ujenzi wa madarasa kwa kushirikiana na jamii.

 Alisema wananchi  wamepewa jukumu la kujenga mpaka msingi na baada ya hapo ofisi ya mbunge ndio inabeba jukumu la kutafuta vifaa vya ujenzi kupitia wadau tofauti wa maendeleo.

Alisema  kupitia Angelina foundation wamekua wakitoa msaada wa matofali ili kuweza kufanikisha ujenzi wa miundombinu.

Amesema mpaka sasa wilaya ya Ilemela ambapo mpaka sasa imeshatoa zaidi ya matofali 40,000 huku idadi ya madarasa ipatayo 176 yakiendelea kujengwa kwa kushirikisha uongozi wa wilaya, wananchi wa ilemela pamoja wa wadau wa maendeleo mkoani Mwanza.