Polisi yaua majambazi wawili Kagera


Na Clavery Christian Bukoba.

Watu wawili wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na polisi wilayani Ngara mkoani Kagera kufuatia majibizano ya risasi na askari polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa Siku mbili kabla ya tarehe 17/04/2019 jeshi la polisi wilayani Ngara lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna majambazi wanajiandaa kufanya uhalifu na kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi wawili waliotambulika kwa majina ya Karimu Abdallah mwenye umri wa 18 raia wa Burundi na mkulima mkazi wa kinyami mkoa wa Giteranyi nchini Burundi na Razalo Silvanusi mwenye umri wa miaka 20 mhangaza mkulima mkazi wa kitongoji cha ngoma mtanzania wakiwa na silaha moja aina ya AK 47 yenye namba UC 8394 na magazini mbili Moja ikiwa na risasi 18 na nyingine ikiwa na risasi 16.

Kamanda Malimi amesema kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa walikiri kujihusisha na matukio kadhaa ya uporaji wa kutumia silaha na kwamba wanakikundi kinachomiliki silaha mbili za kivita ambazo wanazitumia kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali  ambapo walidai moja inatunzwa porini na wenzao ambapo mnamo tarehe 17/04/2019 majira ya saa 5:00 wakati polisi wanaongozana na watuhumiwa kwenda kwenye pori la Rumasi ambako walieleza kuwa wamewaacha majambazi wenzao watatu kutoka nchi jirani ya Burundi wakiwa na risasi na mabomu na gafla baada ya kufika katika pori la Rumasi walianza kushambuliwa na risasi na wao wakajitetea na matokeo yao watuhumiwa waliokuwa nao ambapo walikuwa mbele ya msafara kujeruhiwa vibaya na askari mmoja mwenye namba G. 632 D/C DEOGRATIUS aliyekuwa amevaa bodyharmer.

Kamanda Malimi amesema kuwa askari huyo alikimbizwa hospitali ya nyamiaga wilayani Ngara ambapo alipatiwa matibabu na kuruhisiwa baada ya hali yake kuwa vizuri  na baada ya mashambulizi kuwa makali majambazi walikutwa porini walitokomea kusikojulikana ndani ya pori hilo na eneo la mashambulizi kulikutwa maganda tisa ya risasi na mfuko wa plastiki uliokuwa na risasi 20 za silaha ya AK 47 na majambazi waliojeruhiwa katika mapambano walipopelekwa hospitali walikutwa wamekufa na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani ngara.