Rais Magufuli awaomba Viongozi wa dini kuwaombea Watanzania waache kulalamika


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe amewaomba Viongozi wa dini waendelee kuwaombea Watanzania wachape kazi na waache kulalamika.

Rais Magufuli amesema kuwa waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu na kuwaombea Watanzania kutobaguana.

"Viongozi wa dini nawashukuru sana, endeleeni kuliombea taifa kujenga amani na utulivu, waombeeni Watanzania wachape kazi waache kulalamika, waombeeni Watanzania tusibaguane kwa dini, rangi au makabila," amesema leo Rais Magufuli wakati akizndua Mji wa Serikali jijini Dodoma.