Rais wa TFF ajibu tuhuma za kupokea rusha ya Tsh. Milioni 46 kutoka kwa Rais wa CAF



Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Wallece Karia amekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao kuanzia jana kuwa alipokea rushwa ya Tsh. Milioni 46 kutoka kwa rais wa shirikisho la soka barani Afrika kwa hivi sasa, Ahmed Ahmed ili aweze kumuunga mkono katika uchaguzi wa shirikisho hilo.

Karia akizungumza kwa njia ya simu na Television ya taifa (TBC) amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwasababu yeye hakuwepo madarakani wakati uchaguzi wa CAF unafanyika na kumuweka Ahmed kwenye kiti cha urais.

"Kwanza kwenye mitandao hiyo ambayo ina-trend haijataja jina langu imesema Tanzanian FA president, lakini watu wamitandao ya Tanzania wamebadilisha wameweka jina langu, lakini kipindi hicho wakati Ahmed Ahmed anaingia kwenye uchaguzi mimi sikuwa rais, na nna uhakika pia kwasasabu ukisoma ule mtandao unasema huyo rais wa shirikisho hakupata hiyo hela’’ amesema Karia.

Aidha, Karia ameongeza kuwa kilichopelekea jina lake kutajwa kwenye sakata hilo ni chuki binafsi za watu wanaopingana na utendaji wake wa kazi ndani ya Shirikisho hilo.