Sarri ajipanga kumbakisha Covasic Stanford Bridge


Meneja wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri amekiri kuwa anatamani kumbakisha kiungo wake raia wa Coratia, Mateo Covasic baada ya muda wake wa mkopo kumalizia.

Sarri amesema kuwa ana tatizo katika eneo lake la kiungo na anavutiwa na wachezaji ambao wako vizuri kiufundi hivyo anatamani Chelsea imsajiri Covasic moja kwa moja.

Kiungo huyo kwasasa anaitumikia klabu ya Chelsea kwa mkopo kwa muda wa mwamka mmoja akitokea katika klabu ya Real Madrid.

Mkataba wa mchezaji huyo kuitumikia Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu.