.

4/15/2019

Sera ya ugatuzi wa madaraka kuondoa migogoro katika uongozi


Na. Rahel Nyabali, Tabora

Baadhi ya wadau kutoka mikoa ya Tabora , Kigoma , Katavi na Shinyanga wamesema Sera ya Ugatuzi wa madara itasaidia kuimarisha utendaji kazi na kuondoa muingiliano wa kiutendaji baina ya wanasiasa, watendaji wa serikali na sekta binafsi  jamba ambali litasaidia kuleta maendeleo katika jamii.


Yameelezwa hayo katika kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau juu ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuzi wa madaraka kilichofanyika mkoani Tabora kikihusisha wadau kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga   na Katavi ambapo wanatumia fursa hii kuzungumzia sera itakabvyoleta tija  kwa jamii.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Nodfrey Ngupulaa amesema sera hii itasaidia kila mtu kuwajibika kulingana na nafasi jambo ambalo litasaidia miradi ya serikali kukamilika kwa wakati,

“Sera hii itakapo kamilika itaweza kuondo migogoro katika uongozi wa serikali nah ii itasaidia kila mtu kuifanya kazi kwa ufanisi nahii itasaidia  kuendana na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli,’’, Amesema Ngupula.

Wataalamu kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI akiwemo Juma Rashidi Kaimu mkuu wa Idara ya uratibu wa sekta TAMISEMI amesema  wanaendelea kutekeleza jukumu la kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kupitishwa kwa sera hiy

“Wadau wote watakapo shiriki kutoa maoni itasaidia  kilamtu kufanya kazi  bila muingiliano na  sera hii hailengi sekta Fulani inaangalia sehemu zote kwahiyo nilazima hii lasimu kila mwananchi ashiliki kuikamilisha kwa kutoa maoni," Amesema Rashidi.

Kuwepo mchakato wa upatikanaji wa sera ya Taifa ya Ugatuzi wa madaraka kumetokana  na tathmini iliyofanywa na serikali mwaka 2017 ilionesha kuendelea  kupungua  kukubalika kwa huduma zinazotolewa na tasisi za serikali ikilinganishwa na miaka ya nyuma.