Serikali haijazuia ripoti ya IFM - Waziri Mpango


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameleza kuwa Serikali haijazuia ripoti ya IMF kama inavyoelezwa bali ipo katika majadiliano juu ya maoni ambayo serikali imeyawasilisha IMF kabla ya kuchapishwa kwa ripoti hiyo .

Akijibu swali la Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka leoalietaka kujua  kwa nini Tanzania imezuia uchapishaji wa taarifa hiyo?, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema Serikali haijazuia kuchapishwa kwa ripoti hiyo bali inaendelea na mazungumzo na IMF.

Mwakajoka aliibua hoja hiyo alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Waziri Mpango ameeleza kuwa suala la kawaida na taratibu za IMF kuwasilisha rasimu serikalini kwa maoni kabla ya kuchapisha ambapo serikali husika inakuwa na siku 14 za kujadili na kutoa maoni yake.

Waziri Mpango amesema kuwa IMF haijazingatia maoni ya Serikali ya Tanzania lakini bado mazungumzo yanaendelea.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa baada ya IMF kuijuza dunia tangu Aprili 17 ilipotoa taarifa kuwa baada ya kikao chake, Serikali ya Tanzania, imezuia kuchapisha tathmini iliyofanywa wala kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.