Serikali yaombwa kupeleka huduma za mawasiliano Kata ya Simbay


Na. John Walter, Hanang

Imeelezwa kuwa Wanafunzi wengi  wanaoishi kwenye  Magheto hasa  watoto wa kike wapo kwenye  hatari  ya kukutana na vishawishi vingi hali inayowapa ugumu kumaliza masomo yao.

Hayo yameelezwa na Afisa tarafa wa Simbay Bwana Malamsha wakati akizingumza na wakazi wa kata ya Simbay kwenye mkutanob wa hadhara wa mbunge Dr. Mary Michel Nagu, ambapo amesema kujengwa kwa mabweni ya shule itawanusuru bwanafunzi wengi haswa wa kike na hatimaye kufikia ndoto zao za kuhitimu elimu yao ya sekondari na kuendelea na elimu ya juu.

 Amesema Changamoto kubwa ambayo ipo haswa kwenye shule ya Sekondari ya  kata ya Simbay ni ukosefu wa Mabweni kwa ajili bya wanafunzi ambao wanatoka vijiji mbalimbali kuja kupata elimu hali inayohatarisha usalama wao haswa wanafunzi wa kike.

"Wewe kwa sifa yako tuliokupa ni Simba Jike,una uwezo wa kufanya kazi na una uwezo wa kuangalia shida tulizonazo na ukasaidia,kwa hiyo naomba utusaidie"alisema Malamsha.

Aidha amesema changamoto nyingine ni bara bara ya kutoka Simbay kwenda Gidahab ambayo haipitiki wakati wote na katika kipindi cha mvua ndio hali inakuwa mbaya zaidi hivyo mbunge aweze kuishugulikia ili wanakijiji wafanye shuguli zao kwa urahisi.

Kwa upande mwingine Afisa tarafa huyo amemuomba mbunge kuwashawishi wanaohusika na mitandao ya simu ili wajenge minara  katika tarafa hiyo kwa kuwa maeneo mengi yanakabiliwa na changamoto ya kukosa mawasiliano ya uhakika ya simu hali inayochangia kushindwa kuapata taarifa mbalimbali na kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki.

Naye mbunge wa jimbo la Hanang' Dr.Mary Michael Nagu amesema changamoto zote hizo atazipeleka bungeni kwa kuwa Chama cha mapinduzi kina ushirikianop mzuri na serikali hayo yote yatashugulikiwa.

Mbunge huyo amesema tangu aingie madarakanai anajivunia mengi aliyoyafanya ikiwemo kukarabati miundo mbinu ya elimu huku mheshimiwa Rais Magufuli akiweka msisitizo na mkazo elimu kuwa bila malipo.

Kata ya  Simbay iliyopo wilaya ya Hanang' mkoani Manyara ina jumla ya kaya 1283.