Sijawahi kusaini mtu anyongwe ila... - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hajawahi kusaini mtu anyongwe ila ikitokea kesi ya mauaji ya mtoto akaletewa asaini inawezekana akamuomba Malaika wake amruhusu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mkoani Njombe ambapo amesema kuwa atamuomba Malaika wake amaruhusu asaini kwasababu suala la mauaji ya watoto Mkoani humo limeutia doa Mkoa.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Wabena na Wakinga msiamini ushirikina.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli inakuja baada ya kupotea, kuuawa  kwa watoto 7 Mkoani humo.