Sina mashaka na mechi zinazofuata kwenye ligi kuu - Kocha wa Man U


Meneja wa timu ya Manchester United, Ole Gunnar Solkskjaer, ameeleza kuwa hivi sasa hana presha na mechi zake tatu zinazofuata za Ligi Kuu England kwani anaimani na kikosi chake hakitamuangusha.

Manchester United walitolewa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 4-0 sasa wameelekeza nguvu zao kwenye mechi za Ligi Kuu England.

"Sina mashaka na mechi zinazofuata kwenye ligi kuu kwa sasa nina imani na kikosi changu tupo tayari kupambana hasa kwa mechi zetu tatu zinazofuata," amesema.

Mechi tatu zinazofuata kwa Manchester United ni pamoja na ule dhidi ya Everton utakaopigwa Aprili 21 Jumapili, Manchester City itakuwa ni Jumatano ya Aprili 24 na wa mwisho kati ya hiyo mitatu anayoipigia hesabu ni dhidi ya Chelsea Jumapili , Aprili 28.