Treni ya mizigo yapata Ajali Morogoro


Treni ya mizigo iliyobeba shehena ya ngano iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Mkoani Mwanza imepata ajali Usiku wa kuamkia Aprili 13 mwaka huu, eneo la Kola Manispaa ya Morogoro na kusabaabisha treni nyingine za abiria kushindwa kupita.

Mkuu wa kituo cha Treni Morogoro Bw Salvatory kimaro wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa treni hiyo ilikuwa na injini namba C261 inajumla ya mabehewa 20, kati ya hayo mabehewa matano ya nyuma yaliacha njia na kuanguka, hivyo chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu kama anavyobainisha

Aidha kimaro amefafanua kuwa kuhusu treni za abiria zilizokuwa zikitokea Dar es Salaam kuelekea Kigoma, Mpanda na Mwanza zilifika mapema Morogoro jambo ambalo limesaidia kubadilishwa kwa abiria.