Tupo tayari kukabiliana na matishio yoyote yanayojitokeza - Jenerali Mabeyo


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali  Venance Mabeyo amesema kuwa hali ya usalama kwenye nchi ni shwari na wakati wote wapo tayari kukabiliana na matishio yoyote yatakayojitokeza.

Jenerali Mabeyo ameeleza hayo leo wakati wa hafla ya  uzinduzi wa mji wa kiserikali uliojengwa Ihumwe mkoani Dodoman ambao unazinduliwa  na Rais wa Tanzania, John  Magufuli.

“Hali ya usalama kwenye mipaka yetu ni shwari, ndani ya nchi yetu JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vya wengine liko tayari kuwalinda wananchi na mali zao, wakati wote tupo tayari kukabiliana na matishio yoyote yanayojitokeza," amesema.

Kuhusu ujenzi wa nyumba na ofisi za Serikali, Jenerali Mabeyo amesema kwa kiasi kikubwa kazi hiyo imefanywa na vijana wa JKT na imefanyika kwa miezi mitano.