Ukiwa upinzani Mbunge unakuwa ndio kila kitu, CCM kazi imekuwa nyepesi - Gekul


Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini, amesema kuwa alipokuwa upinzani (CHADEMA), Mbunge unakuwa ndio kila kitu katika majukumu.

Gekulu amesema alipohamia CCM, mambo yanakwenda vizuri na kazi imekuwa nyepesi sana kwasababu kuna mgawanyo mzuri wa kazi na kila kiongozi anafanya majukumu yake.

”Huko nilikotoka Mbunge ndio kila kitu wewe ndiyo mwenyekiti, wewe ndiyo mwenyekiti wa mtaa, wewe ndiyo katibu, wewe ndiyo everything, lakini huku nimeona kwamba kuna system ya chama majukumu ya kichama yanafanyika zaidi na viongozi wa chama” amesema Gekul.

Gekul alisema ”Nilivyohamia CCM nimepata ushirikiano wa hali ya juu sana masuala ya wananchi yanakwenda vizuri sana mwanzoni nilivokuwa mbunge wa upinzani vitu vingi manake nisukume mwenyewe  vinaweza visitekelezwe au visifanyike, lakini sasa hivi nipo CCM mambo yamekuwa rahisi sana.”