UVCCM watakiwa kuchangamkia asilimia 10 ya Fedha za maendeleo


Na John Walter-Babati.

Kutokana na utekelezaji wa Sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) Vijana Wilayani Babati wametakiwa kuchangamkia fursa ya Fedha za maendeleo asilimia 10% zinazotolewa na Serikali ili kuweza kuanzisha miradi itakayowakwamua  kiuchumi

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapindizi Babati Vijijini (UVCCM) Stanley Charles akizungumza katika Baraza la Umoja wa Vijana wa chama hicho ambapo amesema atahakikisha vijana wananufaika na Sera nzuri zinazotokana na Chama cha hicho.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Jitu Soni akifunga baraza hilo la vijana amewahakikishia kuwa fedha zipo ila wanachotakiwa kufanya  wajiunge katika vikundi na wawe na mradi walioanzisha si kuanzisha kwa fedha hizo watakazoomba kupatiwa na serikali.

Naye Afisa utamaduni na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Beatrice Marseli amesema katika mwaka wa fedha 2018-2019 wametoa kiasi cha sh,Mill 57 mikopo kwa Vijana isiyo na riba ili waweze kujiajiri na Kumshukuru Rais Magufuli.

Kwa upande wao mmoja wa Vijana katika baraza hilo Fatuma Abdillahi  ameelezea kuwa  ni fursa nzuri kwao na nafasi bora ambayo vijana wanapaswa kuichangamkia hivyo wapo tayari kuitumia vizuri ili waweze kujikwamua kichumi.