Unapo iba vifaa vya barabarani si kwamba unaikomoa Serikali - Kamanda John


Na Raheli Nyabal, Tabora.

Zaidi ya shilingi milioni tatu zimetumika ili kununua betrii la kuongozea taa za barabarani lililoibiwa katika makutano ya Barabara ya Isevya Mkoani Tabora, jambo ambalo limeisababishia hasara  Serikali ili hali fedha hiyo ingetumika kwa maendeleo mengine.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani TANROADS Raphael Mlimaji na kusema kuwa wizi wa betrii hilo limesababisha kusimama kwa kutumika taa katika eneo hilo jambo ambalo linasababisha ongezeko la ajali Barabarani.

“Hii hasara imesababishwa na mtu mmoja lakini inaathiri wananchi, kati yetu wanafahamu nchi inataka kusonga mbele mnarudisha nyuma nikinyume cha sheria’’ amesema Mlimaji.

 Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tabora John Mfinanga amesema kila Mwananchi awe mlinzi wa mwenzake ili kuweza kuwafikisha wahalifu kwenye Vyombo husika ili kuweza kuimarisha usalma katika jamii.

 “Unapo iba vifaa vya barabarani si kwamba unaikomoa Serikali bali unakomoa wananchi wote nivyema tushirikiane kuwafichua wezi hawa kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya mkoa wetu’’ John  amesema

Aidha kamanda wa usalama Barabarani amewataka wananchi mkoani Tabora kufuata shiria za Barabarani jambo ambalo litasaidia kuondokana na ajali za mala kwa mala.