VIDEO: 'INASIKITISHA' watoto wenye ulemavu wa mgongo wahitaji msaada



Watoto wawili Shedrack Gustav [5] na Jeremia Gustav[2] wakazi wa Mtaa wa Hala mjini Babati wenye ulemavu wa mgongo hali inayowafanya kudumaa, wanaomba watu wenye mapenzi mema waweze kuwasaidia kupata matibabu ili waweze  kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.

Watoto hao wanatakiwa kunyooshwa mgongo kwani tatizo hilo linawafanya wapumue kwa shida.

Baba mara baada ya kuona hali ya watoto ni mbaya aliamua kutoroka na kukimbilia mkoani Dodoma na kumuacha Mwanamke na akiendelea kutafuta namna ya kuwatibu wanae.


Mama huyo Anastazia ameimbia Muungwana Tv kuwa amefanikiwa kupata watoto nane ambao wameshafikisha umri wa kujitegemea.
Mama huyo anasema hali ni mbaya,mvua ikinyesha nyumba inavuja.
Anaomba msaada kwa yeyote atakaeguswa ili aweze kuwapatia watoto hao matibabu.


Kwa yeyote atakaeguswa anaombwa kuwasiliana na mwalimu Peter  Sanka kwa Namba za Simu 0782129598- 0763913797

Mratibu wa kutekeleza Mpango wa taifa wa kutokemeza Ukatili kwa wanawake na watoto mkoa wa Manyara Anna Fissoo akiongozana na wajumbe Felix Erca pamoja na mwalimu Peter Sanka waliamua kufunga safari hadi mtaani hapo wakiwa wameongozana na mwandishi wa Muungwana Tv.

Anasema  tatizo lilianza kwa mtoto Shedrack ambapo alipokuwa alipofikisha umri wa kukaa kila akijaribu kumkalisha inashindikana  ndipo alipoamua kwenda hospitali ambapo aliambiwa mtoto huyo anaonekana aliangushwa,lakini cha kushangaza na kwa mtoto wa pili tatizo likawa kama la
mwenzake

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USIKOSE KU-SUBSCRIBE