Vyama vinne vya upinzani vyamtaka Spika wa Bunge kujiuzulu


Vyama nane Vya Siasa nchini vimemtaka Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kujiuzulu kufuatia sakata baina ya Bunge na CAG kutokana na kusababisha mgongano baina ya Mamlaka na kukwamisha utendaji Kazi.

Mwenyekiti wa UPDP mhe. Fahmi Dovutwa amesema kwa hali ilivyo sasa ya Spika kumtaka CAG kwenda kwa Rais kujieleza ni kuongeza mkanganyiko zaidi unaowaweka wananchi njiapanda juu ya uangalizi wa hesabu za miradi ya maendeleo.

Wakati huo huo vyama hivyo ambavyo ni CHADEMA, CHAUMA, ACT Wazalendo, Democratic Party, CCK na UPDP vimeungana na kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga matumizi ya Sheria ya vyama Vya Siasa ambayo vimedai kuwa inakandamiza misingi ya demokrasia.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema katika kesi yao wameomba mahakama ya Afrika Mashariki kutoa zuio la matumizi ya Sheria hiyo mpaka kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.